Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Hai, mkoani
Kilimanjaro, imesema mtuhumiwa anayedaiwa kutumia jina la Jaji Mkuu
mstaafu, Barnabas Samatta, kutaka kumtapeli Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa, ana kesi ya
kujibu.
Mtuhumiwa huyo ni Abeid Abeid (24), mkazi wa Machame, Hai, mkoani Kilimanjaro.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili, Furahini Kibanga wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani hapa, ulidai kwamba mtuhumiwa alitumia jina hilo la Jaji Mkuu mstaafu, kati ya Aprili na Mei, mwaka 2012 akiwa katika baa ya Florida iliyopo Kata ya Machame kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa Dk. Slaa.
Ilidaiwa kuwa Abeid alimpigia simu Dk. Slaa, akitaka amtumie nauli ya kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo ili awasaidie
Chadema kushinda kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ya kuvuliwa ubunge wake kupitia rufaa namba 47 ya mwaka 2012 iliyokuwa imefunguliwa na Lema dhidi ya Mussa Hamis Mkanga na wenzake wawili. Lema alikuwa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu ya Arusha kumvua ubunge.
Kibanga akiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Denis Mpelembwa, aliieleza mahakama kuwa kesi hiyo imekuja mbele yake kwa ajili ya kutolewa uamuzi mdogo, iwapo mshitakiwa ana kesi ya kujibu au la.
Baada ya kauli hiyo, Hakimu Mpelembwa alisema kwa kuwa upande wa mashtaka umefanikiwa kuwaleta mahakamani mashahidi wanane muhimu,
wakiwamo Jaji Samatta, Profesa Abdalah Safari, Godbless Lema na Dk. Slaa na kujenga hoja za kuishawishi mahakama hiyo, amejiridhisha kwamba Abeid Adam Abeid, ana kesi ya kujibu.
“Mahakama hii, imeona una kesi ya kujibu katika makosa mawili ambayo ni kujifanya Afisa wa Serikali. Alijiita Afisa wa Takukuru, Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro na kosa la pili ni la kutumia jina la Jaji, Mkuu mstaafu, Barnabas Samatta kutaka kujipatia fedha isivyo halali
kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa,” alisema hakimu huyo.
Kosa la kwanza linalomkabili Abeid ni kujifanya afisa wa Serikali, kinyume cha kifungu cha 381 na 302 cha Kanuni ya adhabu, Ibara 16 ya Sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002; na kosa la pili ni kujiita Jaji, Samatta ambalo ni kinyume cha kifungu cha 369 (1) cha Kanuni ya adhabu, Ibara ya 16 ya Sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق