Hakuna
ubishi kuwa Ronaldo na Messi ndio wachezaji bora zaidi duniani, lakini
wenyewe kwa wenyewe katika hali inayoonyesha unafiki wa nafsi zao,
hakuna anayemkubali mwenzake.
Ronaldo
hakumpigia kura Messi wakati wa mchakato wa kura za Ballon d'Or na
badala yake kura zake akapeleka kwa wachezaji wenzake wa Real Madrid
Sergio Ramos, Gareth Bale na Karim Benzema.
Messi
naye akasema “NO” kwa Ronaldo, kura zake mbili akazitupa wachezaji
wenzake wa Argentina Angel di Maria na Javier Mascherano, kura nyingine
akampa Andres Iniesta wa Barcelona. Hata hivyo Ronaldo aliibuka mshindi
kwa mwaka wa pili mfululizo.
Hii
ni janja ya kuogopana, kila mmoja alihofia kumzidishia alama mpinzani
wake, lakini ni wazi kuwa hali hiyo inaporomosha hadhi ya kura za Ballon
d'Or.

Post a Comment