ANGALIA UNAFIKI WA RONALDO NA MESSI KATIKA KURA ZAO ZA MWANASOKA BORA WA DUNIA



Hakuna ubishi kuwa Ronaldo na Messi ndio wachezaji bora zaidi duniani, lakini wenyewe kwa wenyewe katika hali inayoonyesha unafiki wa nafsi zao, hakuna anayemkubali mwenzake.


Ronaldo hakumpigia kura Messi wakati wa mchakato wa kura za Ballon d'Or na badala yake kura zake akapeleka kwa wachezaji wenzake wa Real Madrid Sergio Ramos, Gareth Bale na Karim Benzema. 
Messi naye akasema “NO” kwa Ronaldo, kura zake mbili akazitupa wachezaji wenzake wa Argentina Angel di Maria na Javier Mascherano, kura nyingine akampa Andres Iniesta wa Barcelona. Hata hivyo Ronaldo aliibuka mshindi kwa mwaka wa pili mfululizo.
Hii ni janja ya kuogopana, kila mmoja alihofia kumzidishia alama mpinzani wake, lakini ni wazi kuwa hali hiyo inaporomosha hadhi ya kura za Ballon d'Or.

Post a Comment

أحدث أقدم