"Ulishawahi
kujikuta unatamani kuliko kumtongoza msichana mzuri sehemu
flani japo upate namba yake ya simu ila unajikuta huna jinsi
yeyote au wazo juu ya nini cha kufanya au kuongea, unatamani
kumfata nguvu miguuni zinakua zimekuishia unashindwa hata
kupiga hatua moja kumsogelea, lile wazo pekee la kutaka
kumsogelea linakufanya moyo uwende mbio, mikono iloane na
jasho jembamba kukutoka huku akili yako ikishindwa kufikiria
vizuri nini cha kuweza kuongea iwapo ukimsogelea?."
Unajua nini?,
haipaswi kuwa hivi ndo maana Waulize wanaume ipo kwa ajili yako ilikumaliza maswala madogo madogo kama haya, kukuondoa katika mazingira ya kutokua na maamuzi dhabiti na kutokujua nini cha kufanya ndani ya sekta ya utongozaji na kukufanya uwe mwanaume kiongozi na mtanashati kwa kujua ni nini cha kufanya na mda gani unapaswa kukifanya ili kuwa mtaalamu katika sekta ya mahusiano.
haipaswi kuwa hivi ndo maana Waulize wanaume ipo kwa ajili yako ilikumaliza maswala madogo madogo kama haya, kukuondoa katika mazingira ya kutokua na maamuzi dhabiti na kutokujua nini cha kufanya ndani ya sekta ya utongozaji na kukufanya uwe mwanaume kiongozi na mtanashati kwa kujua ni nini cha kufanya na mda gani unapaswa kukifanya ili kuwa mtaalamu katika sekta ya mahusiano.
Kujiamini
ni kitu kinachochukua nafasi kubwa na ndo msingi mkubwa
katika mahusiano na hasa wakati wa utongozaji, na ndicho
kitu mwanamke hutumia kumpima mwanaume na kumpa nafasi ya
uwezekano wa kuwa na yeye au la, ila mara nyingi mtu
hushindwa kujiamini kutokana na hofu ya kutokujua ni nini
cha kufanya au kuongea wakati wa utongozaji.
Mwanamme
ambaye huwa hafanikiwi kwenye utongozaji hufanya makosa
madogo madogo kama kumpandisha hadhi mwanamke anayemtongoza
mpaka kiasi ambacho anaifanya hadhi yake binafsi kuonekana
ndogo na siyo tu anamtongoza mwanamke kwa wasiwasi na
kutojiamini, bali anamtongoza hovyo hovyo bila mpangilio na
zaidi ya hapo anamuweka wazi mwanamke kwamba anataka
kumjua zaidi ya kawaida na anajitangaza bila kujijua
kwamba, anahitaji na huyo mwanamke apendezwe naye hapo
hapo.
Nayajua
haya kwa sababu kwa muda mrefu na mimi msichana nilikua
hivi hivi nawaona wanaume jinsi wanavyojikanyaga, mtaalamu
wa utongozaji huwa anasubira na huwa hapaparuki hovyo hovyo
tu, kutongoza ni sanaa na inahitaji uelewa mkubwa na hata
mimi iwapo ningelikua ndo huyo mwanamke sidhani kama
ningelikubali hivi hivi, lazima atake kukujua kwanza ndo
mambo mengine yafuate.
Ukitaka
kuishia kusonywa na matusi juu ingia na mstari wa "Dada
samahani nimetokea kukupenda nataka tuwe wote, kila nikikaa
nakuwaza wewe, nikinywa maji nakuona kwenye glasi", bila
kuangalia mazingira na papara za kusema yaliyo moyoni
mwako, huu mstari lazima utakutokea puani, mwanadada ndo
amekuona siku hiyo hiyo, hata alikua hajui mtu kama wewe
upo katika hii dunia, hakujui na unategemea akuambie
anakupenda pia, we vipi?, hapo unapoteza nafasi na utaishia
kuambiwa usiyoyataka na kuumia moyo tu.
Naamini
kabisa mwanaume yeyote mwenye mtazamo sahihi na mwenye
hamu ya kujifunza anaweza kuelewa jinsi ya kutongoza
mwanamke sehemu yeyote na mahali popote pale, kutongoza
hakuitaji kukalili mistari ya kutongozea wala kumpulizia
dawa kutoka kwa mganga, kama unania ya kujifunza endelea
kusoma nakala za waulizewanaume.
Mwanaume
mtongozaji hajishushi na anatumia mbinu ya kuonyesha
ujasiri wa kimaongezi na akiongea na mwanamke, mwanamke
hutambua ya kuwa huyu jamaa ana nia naye kutokana na lugha
anayoitumia wakati wa maongezi.
Makosa
makubwa mawili ambayo hufanya wanaume wakati wa kutaka
kumtongoza msichana, ni kusubiri na kusita kwa muda mrefu
na kutojua nini cha kuzungumza.
Kama ni kwenye sherehe ndipo ulipomuona, piga moyo konde na mwendee na mwambie,
>>"Nimekuona kutoka mbali ila moyo wangu ukang'ang'ania mpaka nije nikusalimie, mambo?"
>>"Siku yako inaendaje?"
>>"Upo upande wa bibi harusi au bwana harusi?"
>>"Oooh,
upande wa bibi harusi, ndo maana dada yako amewahi
kuolewa!, ukoo wenu mzima inavyoonyesha umelaaniwa kwa
uzuri!"
Mchokoze
kwa maneno matamu, muulize maswali ya kumfanya afurahie
maongezi na kama ukiwa unatoa sifa ifiche ndani ya
sentensi inayovutia, ukitaka kumjua uliza maswali ambayo
majibu yake ni mepesi na rahisi, kama ukitaka kujua
anachofanya muulize,
>>"Kwa
hiyo familia nzima mwanafunzi amebaki ni wewe tu, maana
dada yako tayari ameshaolewa?"
Kwa
maswali ya namna hio atajikuta anajiongelea kuhusu yeye
na kukufanya akuzoee mapema, na ukiona maongezi
yanaelekea ukingoni unatakiwa unakuwa shapu na mbunifu
kwa kuanzisha mada nyingine inayovutia zaidi, itakayoleta
maongezi matamu zaidi.
Kujua
kitu cha kusema wakati wa kutongoza ni ngumu, ila
inabidi ujiamini na ufanye kujisahau na kuweka akili kama
upo unaongea na dada yako ila maongezi yaweke yawe ya
kuvutia zaidi na uyapambe kwa sifa bila kuonyesha nia
yako moja kwa moja, mwisho wa maongezi muombe namba ya
simu au omba umtoe mtoko akuonyeshe maeneo hayo maana
wewe ni mgeni na maongezi yamekupendezea na ungependa
kuyaendeleza siku nyingine.
Acha
kuwa na wasiwasi na kufikiria nini cha kuongea, we
mfate kwanza na maongezi yatajitengeneza yenyewe kwa
jinsi ya mazingira mliyopo na weka akilini kitu kimoja,
huyo msichana unayeenda kumtongoza inawezekana
anatongozwa mara tano au zaidi kwa siku tokea alipokuwa
na miaka kumi na nane, kwa hiyo inawezekana
ameshatongozwa zaidi ya mara 1000, kwa hiyo usifanye
vitu ambavyo ameshavizoea kila siku na kuishia kutoa
maamuzi ya kutokubali maombi yako kama wengine
waliokataliwa waliotoa maombi yao hapo mwanzo kabla
yako, kuwa mbunifu na tumia mazingira yako kwa usahihi
na uzuri zaidi.
Hakikisha katika maongezi yako usiongelee wala kugusia vitu vifuatavyo,
- Usimsifie sana, atakuona kama unambeza.
- Usijaribu wala kumuuliza kama ana mtu, ana mshikaji wake au anamahusiano na mtu yeyote yule.
- Usimuulize maswali magumu ambayo yanahitaji uelewa wa kitu fulani.
Vitu vifuatavyo ni ambavyo hutakiwi kuvifanya wakati wa utongozaji,
- Usiongee kwa sauti ya juu sana,
- Usijibu kitu au jambo kwa haraka sana,
- Usiwe unaondoka ondoka au kuhamisha mapozi, usiwe na papara na kuwa mtulivu.
Kitu
cha kuweka akilini zaidi usifikilie sana
unachokiongelea, ukifikiria sana utakaribisha wasi
wasi na kutokujiamini.
Wakati wa maongezi yako ya utongozaji, hakikisha unahusisha mambo yafuatayo,
- Vitu ambavyo anashauku navyo na anavipendelea,
- Vitu ambavyo unashauku navyo,
- Hadithi zenye vichekesho na mguso wa mahaba,
- Jifunze jinsi ya kuhadithia hadithi za kuvutia,
- Mfanye acheke na kutabasamu kwa kile unachokiona,
- Michezo ya furaha na ya kuvutia,
- Unaweza kujikweza kidogo ila usipitilize.

إرسال تعليق