Black
Kopa ni mmoja wa waimbaji wa kiume wa kundi jipya la Ogopa Kopa Classic
Band ambaye amekuja na ladha ya aina yake ya uimbaji.
Ni
mtoto wa malkia Khadija Kopa, mdogo wake na marehemu Omar Kopa, lakini
kwa namna alivyojaaliwa sauti nzuri, hana hata haja ya kusafiria nyota
ya mama yake au kaka yake. Anajitosheleza yeye mwenyewe.
Ukisikiliza wimbo wake “Full Ku-enjoy” utakubali kuwa Black Kopa ni changamoto mpya kwa waimbaji wa kiume wa taarab.
Katika
moja ya mazungumzo yake na Saluti5, Black Kopa ambaye jina lake halisi
ni Muhammed Kibwana, alisema ameingia kwenye ‘game’ kwa miguu yote
miwili na hivyo mashabiki wa muziki wa taarab watarajie mengi kutoka
kwake.
“Full Ku-enjoy” ni utunzi wake Hemed Omar wenyewe wanamwita Sonara wa maneno.
Hebu thibitisha ubora wake kwa kusikiliza hapo chini wimbo wake wa “Full Ku-enjoy”

إرسال تعليق