Askofu: JK asiwaonee aibu watuhumiwa Escrow

Askofu wa Kanisa la Kiluther la Kiinjili Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Tanzania, Amon Kinyunyu.
Askofu wa Kanisa la Kiluther la Kiinjili Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Tanzania, Amon Kinyunyu, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutowaonea aibu na kutofanya kazi ya kindugu na watuhumiwa wote waliohusika katika uchochwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Alitoa kauli hiyo  jana katika ibada ya kuukaribisha mwaka2015 na kusema kwamba kuendelea kukaa kimya kunawapa nafasi ya kutumbua mali za Serikali huku wakiendelea kujisifisha kama vile hawahusiki na tuhuma hizo.

Alisema kwa mwaka huu ambao Rais Kikwete atakabidhi uongozi kwa mtu mwingine hanabudi kutoa maamuzi kuhusu watuhumiwa wa Escrow haraka badala ya kuwatangazia Watanzania ahadi zisizokamilika.

“Tunahitaji 2015  uwe mwaka wa amani, ila kubwa ni Rais wetu asikae kimya kwenye mambo mazito  na kuyafumbia macho,” alisema na

Kuongeza kuwa  Rais anatakiwa kuyatolea maamuzi kwani waliokula fedha hizo wapo mtaani na wanafahamika na wanaendelea kudunda huku wakizidi kulichafua jina lake na kwamba jambo hilo linawaumiza viongozi wa kanisa.

Kuhusu baadhi ya viongozi wa dini kupewa mgawo wa fedha hizo,  alisema jambo hilo lilikuwa la siri kutokana na baadhi yao kuzikuta fedha katika acounti zao, hivyo maamuzi yake yanakuwa na ugumu.

Alisema kuna sadaka za aina mbili ya wazi na siri na baadhi yao walizikuta katika akaunti zao, hivyo siyo dhambi  kwani nia yao ni zifike katika kanisa, ila  tatizo ni zinatoka wapi.
 
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

Previous Post Next Post