Askofu wa Kanisa la Kiluther la Kiinjili Tanzania
(KKKT), Dayosisi ya Tanzania, Amon Kinyunyu, amemtaka Rais Jakaya
Kikwete kutowaonea aibu na kutofanya kazi ya kindugu na watuhumiwa wote
waliohusika katika uchochwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti
ya Tegeta Escrow.
Alitoa kauli hiyo jana katika ibada ya kuukaribisha mwaka2015 na kusema kwamba kuendelea kukaa kimya kunawapa nafasi ya kutumbua mali za Serikali huku wakiendelea kujisifisha kama vile hawahusiki na tuhuma hizo.
Alisema kwa mwaka huu ambao Rais Kikwete atakabidhi uongozi kwa mtu mwingine hanabudi kutoa maamuzi kuhusu watuhumiwa wa Escrow haraka badala ya kuwatangazia Watanzania ahadi zisizokamilika.
“Tunahitaji 2015 uwe mwaka wa amani, ila kubwa ni Rais wetu asikae kimya kwenye mambo mazito na kuyafumbia macho,” alisema na
Kuongeza kuwa Rais anatakiwa kuyatolea maamuzi kwani waliokula fedha hizo wapo mtaani na wanafahamika na wanaendelea kudunda huku wakizidi kulichafua jina lake na kwamba jambo hilo linawaumiza viongozi wa kanisa.
Kuhusu baadhi ya viongozi wa dini kupewa mgawo wa fedha hizo, alisema jambo hilo lilikuwa la siri kutokana na baadhi yao kuzikuta fedha katika acounti zao, hivyo maamuzi yake yanakuwa na ugumu.
Alisema kuna sadaka za aina mbili ya wazi na siri na baadhi yao walizikuta katika akaunti zao, hivyo siyo dhambi kwani nia yao ni zifike katika kanisa, ila tatizo ni zinatoka wapi.

CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق