ZIKIWA
zimepita siku chache tangu mwaka wa 2015 uanze, mwanadada mwenye umbo
matata Bongo, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ amekiri kuuanza vizuri baada ya
kupima ngoma.Akipiga stori na gazeti hili, Anti Lulu alisema anafurahi
kwa kuwa ameuanza mwaka vizuri baada ya kwenda kupima Ukimwi
akiongozana na mama yake na kujikuta yupo salama.
Mwanadada mwenye umbo matata Bongo, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ akipozi.
“Yaani nina furaha ya ajabu baada ya kukutwa niko mzima kwani
nilikuwa na wasiwasi sana kutokana na njia nilizopitia kutokuwa salama,
mama yangu ndiye aliyenishauri na kunisindikiza hospitali, nawasihi
wasanii wenzangu nao wakapime ili wagundue afya zao na waweze kuishi
bila wasiwasi,” alisema Anti Lulu.
Post a Comment