LICHA
ya kushauriwa na daktari kuhusu kutulia na kutovaa viatu virefu
kutokana na ujauzito, mwigizaji Aunt Ezekiel ameonekana kuwa ni sikio la
kufa kwani ameendelea kuvaa kama kawaida.Aunt aliendeleza ubishi huo
Jumatano iliyopita mjini Dodoma alipokuwa amekwenda katika Pati ya Good
Bye 2014 iliyoandaliwa na Kampuni ya Endless Fame ambapo mashabiki
walimshuhudia Aunt akiwa amevaa kigauni kifupi pamoja na viatu virefu
kama kawa.
Hivi karibuni Aunt alishauriwa na daktari mmoja wa Dar aitwaye Chale kutovaa viatu virefu kwani huweza kumsababishia matatizo mtoto aliye tumboni.
Mwigizaji wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
“Mh! Huyu Aunt si kashauriwa apumzike maana tumbo kubwa na asivae viatu virefu, mbona anaendelea sasa?,” alihoji shabiki mmoja.Hivi karibuni Aunt alishauriwa na daktari mmoja wa Dar aitwaye Chale kutovaa viatu virefu kwani huweza kumsababishia matatizo mtoto aliye tumboni.
Post a Comment