Baada ya sokosoko kuu la kwanini?? muda wote huu kijana Nassib
Abdul – Diamond Platnumz pamoja na list yake ndeeeefu ya mabinti wa
bongomovies aliowahi kutembea nao hajawahi kuwa hata na mtoto wa
kusingiziwa, HATIMAYE jana kupitia kwenye nyezo za kiteknolojia tumeweza
kudokezwa juu ya ujauzito alionao mwanadada ZARI
ambao ni fika utakuwa wa kijana huyu anayetamba na wimbo wa “Nitampata
wapi” ambao wachunguziwa mambo wanadai ETi ni dedication kwa mpenzi wake
maarufu wa zamani.
USHAHIDI WA UJAUZITO HUO
Usiku wa jana, Dimaond aliweka ujumbe unaosema “I can not wait to have you on my hands #Chibu_Junior” akimaanisha “siwezi kusubiri kukuweka kwenye mikono yangu #Chibu_Junior” huku
akiambatanisha na picha ya Ultra sound aliyoupiga na Zari (Kama hujui
Ultra sound ni nini Tafadhali google) na baadaye Zari naye akapost picha
yake akichukuliwa vipimo hivyo bila kuandika kitu chochote na kuwaacha
wananchi wakimwagika na comment za kutosha kuhusu picha hizo ambazo fika
zinaonesha wawil hao wanaweza kujaliwa mtoto mwaka huu
Je unafikiri hii inaweza kuwa “Project nyingine” au ni kweli wawili hawa wanatarajiwa kuwa wazazi?? Tupe maoni yako
Post a Comment