MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CCM KWENYE ESCROW..Hii kama inamgusa Profesa Muhongo Vile, si ndiye aliyebaki Kiporo?


Kamati kuu ya halmashauri kuu ya  CCM imeitaka Serikali kuendelea na mchakato wa kutekeleza maazimio yaliyofikiwa na bunge kwa watuhumiwa wote wa kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za akaunti ya Escrow.

Aidha kamati ndogo ya maadili imeagizwa kuchukua hatua za kinidhamu kwa viongozi wenye dhamana ndani ya chama waliojihusisha na kashifa hiyo.

Hayo alisema Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Itikadi na uenezi Nape Nnauye kwenye mkutano wake wa mkutano na waandishi wa habari Kisiwandui alisema kwa upande wa viongozi wa  chama cha mapinduzi waliotajwa katika kashfa ya fedha ya akaunti ya Tegeta Escrow, kamati kuu imeitaka kamati ndogo ya maadili kukaa katika kikao Januari 19  kulichunguza suala hilo na kulitolea maamuzi.

Aliwataja wajumbe hao ambao wanashikilia nyadhifa za juu ndani ya chama cha mapinduzi ni pamoja na Professa Anna Tibaijuka ambaye ni mjumbe wa kamati kuu,William Ngeleja pamoja na Andrew Chenge wote ni wajumbe wa NEC kujipima na kufanya tathmini ya maamuzi.

Nnauye alisisitiza kwamba kamati kuu imesikitishwa sana na sakata la kashfa za fedha
akaunti ya Tegeta Escrow huku ikiwataka viongozi waliopewa dhamana kujenga utamaduni
wa kuwajibika kwa dhamana zao na kuacha kusubiri kuwajibishwa kwa mambo waliyofanya
na wahusika wakuu.

'Hayo ndiyo maamuzi ya kikao cha kamati kuu.....serikali imetakiwa kuendelea na
mchakato wa kutekeleza maazimio ya bunge la jamhuri ya muungano kwa wale wote
waliotajwa katika sakata la Escro.......lakini waliopewa adhabu ya kifungo kufanya
kampeni za urais kabla ya wakati hawa watachunguzwa tena mwezi ujao baada ya adhabu
waliyopewa kukamilika'alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post