Kamati kuu ya halmashauri
kuu ya CCM imeitaka Serikali kuendelea
na mchakato wa kutekeleza maazimio yaliyofikiwa na bunge kwa watuhumiwa wote wa
kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za akaunti ya Escrow.
Aidha kamati ndogo ya
maadili imeagizwa kuchukua hatua za kinidhamu kwa viongozi wenye dhamana ndani
ya chama waliojihusisha na kashifa hiyo.
Hayo alisema Katibu wa
halmashauri kuu ya CCM Itikadi na uenezi Nape Nnauye kwenye mkutano wake wa mkutano
na waandishi wa habari Kisiwandui alisema kwa upande wa viongozi wa chama cha mapinduzi waliotajwa katika kashfa ya
fedha ya akaunti ya Tegeta Escrow, kamati kuu imeitaka kamati ndogo ya maadili kukaa
katika kikao Januari 19 kulichunguza
suala hilo na kulitolea maamuzi.
Aliwataja wajumbe hao
ambao wanashikilia nyadhifa za juu ndani ya chama cha mapinduzi ni pamoja na
Professa Anna Tibaijuka ambaye ni mjumbe wa kamati kuu,William Ngeleja pamoja
na Andrew Chenge wote ni wajumbe wa NEC kujipima na kufanya tathmini ya
maamuzi.
Nnauye alisisitiza kwamba
kamati kuu imesikitishwa sana na sakata la kashfa za fedha
akaunti ya Tegeta Escrow
huku ikiwataka viongozi waliopewa dhamana kujenga utamaduni
wa kuwajibika kwa dhamana
zao na kuacha kusubiri kuwajibishwa kwa mambo waliyofanya
na wahusika wakuu.
'Hayo ndiyo maamuzi ya
kikao cha kamati kuu.....serikali imetakiwa kuendelea na
mchakato wa kutekeleza
maazimio ya bunge la jamhuri ya muungano kwa wale wote
waliotajwa katika sakata
la Escro.......lakini waliopewa adhabu ya kifungo kufanya
kampeni za urais kabla ya
wakati hawa watachunguzwa tena mwezi ujao baada ya adhabu
waliyopewa
kukamilika'alisema.
إرسال تعليق