Muleba. Mkazi mmoja wa Kijiji cha Bushembe,
wilayani Muleba, mkoani Kagera amefariki dunia kwa kujinyonga baada ya
kumpiga mwanaye na kumpasua kichwa.
Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Dickson Wilson
alimtaja mtu huyo kuwa ni Godfrey Joseph, mkazi wa Kijiji cha Bushembe
na kwamba tukio hilo lilitokea Januari 3, mwaka huu.
Wilson alisema kabla ya kujinyonga, alimpiga mtoto
wake wa miaka minane na kumjeruhi vibaya kichwani na kuhisi kuwa
amemuua. Alisema hilo ni tukio la pili kwa marehemu kulifanya la
kujeruhi watu wa familia yake, kwani awali alimpiga mkewe na kumchoma na
spoku ya baiskeli iliyokuwa na moto sehemu zake za siri, kitendo
kilichomfanya mwanamke huyo aondoke nyumbani.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rubya alikolazwa mtoto
huyo kwa matibabu, Modesti Rwakahebula alisema wanaendelea kumtibu na
hali yake bado haijatengamaa.

Post a Comment