Mwanaume
mmoja amefikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji baada ya polisi kudai
kuwa alimtupa mtoto wake mwenye umri wa miaka 5 kutoka juu ya daraja
mjini St Petersburg.
Afisa wa polisi alisema alijionea tukio hilo
la kushangaza baada kumwandama John Jonchuck Jr, mwenye umri wa miaka
25, baada ya kuona akiendesha gari lake kwa kasi, alisema afisaa mkuu wa
polisi Anthony Holloway. Mtoto huyo aliyetupwa ndani ya maji yenye kina cha mita 18 alipatikana akiwa amefariki saa moja baadaye. Polisi hawana uhakika ikiwa mtoto huyo alifariki kabla ya kutupwa ndani ya maji lakini uchunguzi bado unafanywa. Bwana Jonchuck alikamatwa dakika 30 baadaye na alitarajiwa kufikishwa mahakamani Alhamisi. Jonchuck alimtupa mwanawe majini katika hali ya kutatanisha
Holloway alisema afisaa mmoja
wa polisi ambaye alikuwa likizoni alishtushwa na gari lililompita kwa
kasi likiwa likendeshwa kwa kilomita 161 kwa saa na bwana Jonchuck.. Afisaa huyo ambaye hakutambuliwa aliendesha gari lake kwa kasi na kumfuata Jonchuck ambaye alisimamisha gari lake ghafla. Jonchuck
aliondoka kwenye gari lake na kumkaribia polisi na muda si muda
alikwenda upande mwingine wa gari na kumchukua mwanawe, kumkumbatia kwa
muda. Polisi alisema alisikia mtoto huyo akipiga mayowe lakini hakumbuki
vyema kwani muda mfupi baadaye babake mtoto huyo alimtupa ndani ya maji
umbali wa kilomita 2.4 kutoka juu ya daraja hilo. ''Baada ya kitendo chake mshukiwa alitoroka,'' alisema afisaa huyo wa polisi. Nimekuwa
nikiwashika wahalifu kwa miaka 29, lakini sijawahi kujionea kitu kama
hiki sina habari kabisa alichokuwa anakitafakari mshukiwa huyo. Bwana
Jonchuck, anayeishi na babake alikuwa ameruhusiwa na mahakama kuishi na
mwanawe baada ya kukosana na mama ya mtoto huyo. Aliwahi kushitakiwa
kwa kosa la kumchapa mkewe pamoja na kuendesha gari lake akiwa mlevi
mwaka 2013
Post a Comment