Mpwapwa. Mtoto mchanga mwenye umri wa mwezi
mmoja, Yadiko Chigoda amelazwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa
wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma baada ya kupigwa na mchi kichwani na baba
yake mzazi na kumsababishia maumivu makali.
Akizungumza na Mwananchi mama mzazi wa mtoto huyo,
Carolina Mnyawami mkazi wa Kijiji cha Mingui Kata ya Lumuma wilayani
hapa alisema, tukio hilo limetokea jana saa 4 asubuhi wakatimume wake
Fabian Chigoda alipokuwa akipigana na kaka yake kwa kuchapana fimbo na
yeye aliamua kuwaamulia ugomvi huo.
“Nilipowanyang’anya fimbo ili wasiendelee
kupigana, mume wangu aliokota mchi na kunirushia kichwani... Niliukwepa
ili usinipige ndipo ulipompiga kichwani mwanangu niliyekuwa nimembeba
mgongoni,” alisema Carolina.
Aliongeza kuwa, “Baada ya kuona kuwa amempiga mtoto alikimbia na hajulikani alipo mpaka sasa.”
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Said Mawji
amethibitisha kumpokea mtoto huyo na kwamba kwa sasa anaendelea kupatiwa
uchunguzi zaidi wa afya yake.
“Mtoto huyo aliumia sana kichwani lakini bado
tunampatia tiba na uchunguzi zaidi kwenye fuvu la kichwa, kwani
inaonekana kama vile limepasuka.”
Hata hivyo, alisema wanafanya mpango wa kumpa
rufaa mtoto huyo ili aweze kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Dodoma.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mingui, Mwingwa Udoba
alisema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia na kwamba bado
wanamtafuta baba mzazi wa mtoto huyo kwa kuwa alikimbia baada ya tukio
hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alipotafutwa simu yake ilipokewa na mtu aliyesema yuko kwenye kikao cha kazi
Post a Comment