Tabora. Mwenyekiti mmoja wa CCM wilayani Uyui,
(jina linahifadhiwa) anatuhumiwa kumlawiti kijana mmoja nyumbani kwake
maeneo ya Bachu baada ya kumlewesha pombe.
Kijana huyo anayefanya biashara ya kuuza chipsi
eneo la Bachu, Manispaa ya Tabora anadaiwa kulawitiwa na mwenyekiti huyo
wiki iliyopita kisha kuingiziwa vitu kwenye makalio yake.
Mmoja wa ndugu za kijana huyo, alikiri kwa ndugu yake kufanyiwa vitendo visivyofaa baada ya kuleweshwa pombe.
Kutokana na tukio hilo, ndugu huyo alimpigia simu
mwenyekiti huyo kumuulizia kuhusu tukio hilo lakini alikana na waliamua
kutoa taarifa polisi.
Alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo, mtuhumiwa
alikanusha kuhusika na kitendo hicho na kwamba ni mahasimu wake wa
kisiasa ndiyo wametengeneza tukio hilo kwa lengo la kumchafua kisiasa.
Alisema hamfahamu kabisa kijana huyo na hawezi kufanya kitendo hicho, kwani ni kiongozi anayeheshimika kwa jamii.
“Kwanza huyo kijana kwa kweli simfahamu na haya ni
mambo ya kutengenezwa na baadhi ya mahasimu wangu kisiasa,” alisema
mtuhumiwa huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Susan Kaganda
alithibitisha taarifa za tukio hilo kufikishwa kituoni na wanachunguza
iwapo lina ukweli. “Taarifa hizi zimefika kwetu na sisi kila tuhuma
tunaifanyia kazi,” alisema KamandaKaganda. Taarifa kutoka ndani ya
polisi zilidai kuwa maofisa wa jeshi hilo kutoka makao makuu Dar es
Salaam wamewasili mjini hapa kufuatilia tukio hilo.
Baadhi ya viongozi wa CCM Wilaya ya Uyui,
walikwenda polisi kufuatilia suala hilo baada ya mwenyekiti wao
kukamatwa na kuhojiwa kutokana na tukio hilo.
Mmoja wa viongozi hao ambaye hakupenda kutajwa
jina lake, alisema hawapendi kuingilia suala hilo na wanaviachia vyombo
vya dola vifanye kazi yake.

Post a Comment