BABA WA KIPA WOJCIECH SZCZESNY AWACHARUKIA MABEKI WA ARSENAL …asema hawana msaada kwa mlinda mlango

Szczesny left his goal unattended before Sadio Mane converted from a tight angle for Saints' first
Maciej Szczesny baba wa kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny amemtetea mwanae kuafuatia makosa aliyofanya katika mechi dhidi ya Southampton siku ya mwaka mpya huku mlinda mlango huyo akiruhusu mabao mawili bila majibu.
Baba huyo ambaye naye aliwahi kuwa kipa wa timu ya taifa ya Poland, amewashutumu vikali mabeki wa Arsenal kwa kusema msaada wao kwa mwanae ulikuwa ni sifuri.
Akizungumza na gazeti la michezo la Przegladu Sportowego, Maciej Szczesny alimlinganisha beki Per Mertesacker na kifaru.
“Ni kweli mwanangu alifanya kosa katika goli la kwanza lakini kwa namna mabeki wa Arsenal walivyocheza ilikuwa ni kituko, hakuna mtu aliyesumbuka kusaidia,” anaeleza Maciej Szczesny.
“Laurent Koscielny alistahili kukimbia na kwenda kumsaidia kipa, Per Mertesacker naye alipaswa kusimama golini.

“Lakini kwa mshangao wa wengi, hawakufanya hivyo na msaada wao kwake ukawa ni sifuri.”

Post a Comment

Previous Post Next Post