
Maciej
Szczesny baba wa kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny amemtetea mwanae
kuafuatia makosa aliyofanya katika mechi dhidi ya Southampton siku ya
mwaka mpya huku mlinda mlango huyo akiruhusu mabao mawili bila majibu.
Baba
huyo ambaye naye aliwahi kuwa kipa wa timu ya taifa ya Poland,
amewashutumu vikali mabeki wa Arsenal kwa kusema msaada wao kwa mwanae
ulikuwa ni sifuri.
Akizungumza na gazeti la michezo la Przegladu Sportowego, Maciej Szczesny alimlinganisha beki Per Mertesacker na kifaru.
“Ni
kweli mwanangu alifanya kosa katika goli la kwanza lakini kwa namna
mabeki wa Arsenal walivyocheza ilikuwa ni kituko, hakuna mtu
aliyesumbuka kusaidia,” anaeleza Maciej Szczesny.
“Laurent Koscielny alistahili kukimbia na kwenda kumsaidia kipa, Per Mertesacker naye alipaswa kusimama golini.
“Lakini kwa mshangao wa wengi, hawakufanya hivyo na msaada wao kwake ukawa ni sifuri.”
إرسال تعليق