Walikwenda
mkoani Mbeya na bendi yao Rungwe Music Band (zamani Wana Extra), bendi
ikasambaratikia huko kila mtu akarejea Dar na hamsini zake, Banza
akaamua kwenda Tunduma na huko ndiko balaa lilipomkumba.
Pengine
bado uko kizani. Ni kwamba mwanamuziki nyota wa dansi Ramadhani Masanja
“Banza Stone” yuko mahututi mjini Tunduma na hana huduma yoyote ya
kimatibabu.
Kwanini
Tunduma? Bendi yao ya Rungwe ilikuwa na ziara katika miji kadhaa ya
mkoa wa Mbeya, ziara ambayo haikuwa na mafanikio, jambo
lililowalazimisha wanamuziki wa bendi hiyo kurejea jijini Dar es Salaam
bila utaratibu maalum.
Wakati
baadhi ya wanamuziki wengine wakirejea Dar es Salaam kwa msaada wa mdau
wa muziki wa Mbeya mjini Yussuf Fitina, Banza Stone yeye pamoja na
wanamuziki wengine wawili akaamua kwenda Tunduma kwa mdau mwingine wa
mjini humo anayefahamika kama Brother K, kwa bahati mbaya Banza
hakumkuta mwenyeji wake.
Kwa
hali hiyo Banza akaanza kuishi maisha ya kubahatisha hapo Tunduma huku
ikidaiwa pia kuwa alikuwa akitumia kilevi kwa sana tu, wanamuziki
aliokwenda nao huko wakaondoka na kumwacha peke yake ugenini.
Katika
siku mbili zilizopita, hali ya Banza ikabadilika, akaanza kuugua,
nyumba ya wageni aliyofikia nayo ikamkataa, lakini msamaria mmoja
mwanadada anayejitaja kwa jina moja la Nana akabeba jukumu la kumhudumia
Banza (japo si kwa kumpeleka hospitali).
Nana amemchukulia Banza chumba katika nyumba ya wageni yenye jina la Palace Lodge.
Katika
mazungumzo ya njia ya simu kati ya Nana na mdau wa muziki wa dansi Deo
Mutta Mwanatanga wa Dar es Salaam ambayo Saluti5 imefanikiwa kapata
‘clip’ ya maongezi hayo, ni kwamba hali ya Banza inazidi kuzorota badala
kuimarika.
“Hali ya Banza si nzuri, leo jioni (jana) alitapika sana na kudondoka,” ilisema sehemu ya mazungumzo hayo ya Nana.
Aidha,
katika mjadala mwingine wa wadau wa muziki kupitia makundi ya Whatsapp,
Saluti5 ilifanikiwa kupata sehemu ya maelezo ya mtu anayeitwa Rahim
ambaye ni kama mtoto wa nyumbani kwa kina Banza – ni ndugu wa hiyari.
Rahim
alieleza kama ifuatavyo: “Naitwa Rahim ni mdogo wa Banza kifamilia. Sie
ndiye tulikuja nae na band ya Rungwe huku Mbeya, akaniaga kuwa
anakwenda Tunduma kuonana na Brother K. “Hali ya Banza ilianza
kubadilika tangu yupo Kyela baada ya kuibiwa begi lake lililokuwa na
vidonge vyake vya dozi lakini akagoma kuduri Dar,” ndivyo ilivyosema
taarifa hiyo ya Rahim. “Kwa sasa mimi niko Mbozi, lakini kesho (leo)
mapema nitakuwa Tunduma, najua jinsi ya kuwaelewesha madaktari ili Banza
apate matibabu,” iliendelea taarifa ya Rahim.
Kwa
mujibu wa Rahim ni kwamba Banza haruhusiwa kupata dawa (za kifua kikuu)
hadi kwenye kituo aliachoandikiwa dozi hiyo – Dar es Salaam.
Akiongea
na Saluti5, Deo Mutta akasema Nana ameombwa ahakikishe anamsafirisha
Banza hadi Mbeya mjini na hapo mipango ya kumrejesha Dar es Salaam
itafanyika chini ya mdau Yussuf Fitina.
Hii
si mara ya kwanza, wala ya pili, wala ya tatu kwa Banza Stone kuugua
hadi kuwa mahututi, lakini bado tatizo sugu la mwanamuziki huyo mwenye
washabiki wengi ni kutozingatia masharti ya madktari.
Banza
anatakiwa kupumzika, kupata lishe ya maana, kuepuka pombe na vileo
vingine lakini vyote hivyo kwake ni vitu visivyowezekana.
إرسال تعليق