BARCELONA YACHARUKA, YAPIGA 5 - 0 - Messi, Suarez, Neymar wote wacheka na nyavu


Kulikuwa na mashabiki 27,099 waliojitokeza uwanjani lakini mahudhurio hayo machache kwa Barcelona kuliko yoyote yale msimu huu, yakashuhudia timu yao ikiichakaza Elche 5-0 kwenye mchezo wa kombe la Copa del Rey.
Uwanja wa Nou Camp wenye uwezo wa kubeba watu 98,000 ukawa shuhuda wa kisago kwa timu inayoburuza mkia La Liga huku kocha wa Barcelona, Luis Enrique akipanga kikosi cha nguvu tofauti na mechi yao waliyofungwa 1-0 na Real Sociedad.
Luis Enrique anapigania kibarua chake kilichoko mashakani na sasa ni wazi kuwa timu yake tayari imepenya hatua ya robo fainali ambapo itavaana na mshindi kati ya Atletico Madrid na Real Madrid.
Messi, Neymar na Luis Suarez wakaunda safu tishio ya ushambuliaji na wote wakafunga katika kipindi cha kwanza.
Neymar ndiye aliyekuwa kijogoo zaidi kwa kufunga mabao mawili huku goli lingine likifungwa na Jordi Alba

Post a Comment

Previous Post Next Post