Kulikuwa
na mashabiki 27,099 waliojitokeza uwanjani lakini mahudhurio hayo
machache kwa Barcelona kuliko yoyote yale msimu huu, yakashuhudia timu
yao ikiichakaza Elche 5-0 kwenye mchezo wa kombe la Copa del Rey.
Uwanja
wa Nou Camp wenye uwezo wa kubeba watu 98,000 ukawa shuhuda wa kisago
kwa timu inayoburuza mkia La Liga huku kocha wa Barcelona, Luis Enrique
akipanga kikosi cha nguvu tofauti na mechi yao waliyofungwa 1-0 na Real
Sociedad.
Luis
Enrique anapigania kibarua chake kilichoko mashakani na sasa ni wazi
kuwa timu yake tayari imepenya hatua ya robo fainali ambapo itavaana na
mshindi kati ya Atletico Madrid na Real Madrid.
Messi, Neymar na Luis Suarez wakaunda safu tishio ya ushambuliaji na wote wakafunga katika kipindi cha kwanza.
Neymar ndiye aliyekuwa kijogoo zaidi kwa kufunga mabao mawili huku goli lingine likifungwa na Jordi Alba

إرسال تعليق