Stori: Mayasa Mariwata MUUZA
sura kwenye sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ ambaye alikiri
kubanjuka na mastaa wasiopungua 15, amesema sababu zinazomsababisha
asidumu na mwanaume mmoja kwenye mapenzi ni kutokana na mateso
aliyoyapata kwenye ndoa ya utotoni.
Muuza sura kwenye sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’.
Akibonga mawili matatu na paparazi wetu, Bozi alisema tatizo la
kutokuwa na msimamo kwenye mapenzi linatokana na kuumizwa na mwanaume
ambaye alimuamini na kuingia naye kwenye ndoa, ambapo aliambulia vipigo
na mafumanizi ya mara kwa mara.
“Ukweli mshipa wa kupenda umeshanikatika, nikiwa na mwanaume kwa kipindi kifupi tu namchukia na kusitisha uhusiano, chanzo kinatokana na mwanaume ambaye alinibembeleza anioe nikiwa na umri wa miaka 17 tu na kila siku kufuma SMS za wanawake na hata kumshuhudia, nilichoambulia ni mtoto ambaye jukumu zima la malezi ni mimi mwenyewe,” alisema Bozi.
![](http://api.ning.com/files/W8k9GghxLBtpZwEQEw7XSuDSZpwVU5Jr0M3OhY04VhLxNPEhaT3nIBTCpfz2n7a6AHv9sQsAtOkMci1vpbcwpYir3ihvqlvr/IMG20141110WA0007.jpg?width=650)

إرسال تعليق