Aliyekuwa
Gavana wa Florida kupitia tiketi ya chama cha Republican nchini
Marekani Jeb Bush ameripotiwa kujiuzulu kutoka nyadhfa zake zote za bodi
akijiandaa kuwania urais mwaka ujao.
Gazeti la The WashingtonPost
limenukuu ujumbe wake kutoka kwa msaidizi wake uliodai kwamba bwana
Bush pia amejiuzulu katika bodi ya hazina yake ya elimu.
Kiongozi
huyo mwenye umri wa miaka 61 pia alitangaza mwezi uliopita kwamba
alikuwa na wazo la kutaka kuwania wadhfa huo mkuu ambao hapo mbeleni
ulishikiliwa na babaake George Bush na nduguye George W.
Amesema kuwa atafanya uamuzi wa mwisho baada ya kubaini iwapo ana ufuasi wa kutosha.(BBC)
Post a Comment