Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea malalamiko
kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu ushushwaji wa bei za filamu
uliotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment.
Wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei
iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha
tasnia ya filamu kudharauliwa na pia haina tija katika tasnia ya
filamu.
Wizara inaiagiza kampuni ya Steps Entertainment kusitisha kuanza
kuuza filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka hapo muafaka utakapopatikana
katika kikao kitakachofaninya kati ya Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na
Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA HABARI,
VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Post a Comment