STAA
wa Bongo Movies, Halima Yahya ‘Davina’ amekiri kuwa ndani ya tasnia
yao, kuna wasanii wengi wa kike wanajiuza kwa maslahi yao binafsi.
Staa wa Bongo Movies, Halima Yahya ‘Davina’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Davina alisema wasanii wanaofanya
hivyo ni wale wasio na nia ya dhati, wapo kwenye tasnia kwa ajili ya
kuuza sura na kujinadi kwa mapedeshee.
“Tatizo ni kwamba wasanii tumekutana kila mmoja ana tabia zake na ni
ngumu kujua undani wa mtu kwa kumtazama mara moja, sasa utakuta mtu yupo
radhi aombe kucheza filamu hata bure kwa kuamini kwamba ataonwa na
wanaume wenye pesa zao, na kweli inakuwa hivyo kwani wanapowatokea
hawakatai, kimsingi wanatuchafua sana sisi ambao tupo serious na kazi,”
alisema Davina.
إرسال تعليق