Staa wa Bongo Movies, Halima Yahya ‘Davina’.
Stori: Laurent Samatta TAHADHARI!
Staa wa Bongo Movies, Halima Yahya ‘Davina’, amewatahadharisha viongozi
mbalimbali wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye
uchanguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani 2015 kuwa makini ili
wasisababishe vurugu au uvunjaji wa amani.
Davina alifunguka hayo juzikati katika mahojiano maalumu na paparazi
wetu ambapo alisema mwaka huu unakuja kukiwa na changamoto nyingi
kutokana na matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea hivyo viongozi na
Watanzania kwa ujumla wanatakiwa kuwa makini ili kuepuka umwagaji wa
damu.
“Huu mwaka mzito sana na tunaweza kufurahi lakini kumbe kuna baadhi
ya viongozi wanapanga kufanya mambo ya ajabu, tumeona uchanguzi wa
Serikali za Mitaa juzi mambo yalivyokuwa, viongozi na Watanzania
wenzangu lazima tuwe macho na sisi wapiga kura tumpinge kiongozi yeyote
atakayetaka madaraka kwa njia ya vurugu,” alisema Davina.
Post a Comment