Mwigizaji wa filamu Bongo Jacqueline Wolper.
KIMENUKA!
Mwigizaji Jacqueline Wolper ameibua tafrani la aina yake kwa Mbongo
Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kumtumia meseji
iliyomtia shaka mpenzi wa staa huyo, Siwema.
Tukio
hilo lilitokea juzikati nyumbani kwa Nay wa Mitego, Kimara- Korogwe
jijini Dar ambapo ilisemekana Wolper alituma SMS iliyokuwa ikiuliza
muafaka wa jambo fulani ndipo Siwema akaja juu na kuanza kumcharukia
bebi wake huyo.

Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa na mpenzi wake Siwema.
Alipoulizwa Nay wa Mitego kuhusiana na ugomvi huo, alifunguka:
“Wolper
ni rafiki yangu kitambo, ni mtu wangu tunayeelewana kupita maelezo,
hivyo juzikati nilikuwa nikichati naye juu ya kutaka kumshirikisha
kwenye video ya wimbo wangu mpya wa Akadumba, Siwema dizaini kama
alimaindi kuona nawasiliana naye lakini nilimuelewesha na kila kitu kipo
sawa.”

Post a Comment