Duh! Kama ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali wawili wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba, limekwisha, basi umenoa baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana.
Baadhi ya wasanii wa Bongo fleva wakiwa kwenye mkutano.
Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree Hilton
jijini Dar, juzikati ambapo wasanii mbalimbali walikutanishwa na kampuni
moja ya huduma ya simu za mkononi ili kuzungumza na wanahabari juu ya
maandalizi ya tamasha.
Waandishi wetu, wakiwa wameingiwa na roho ya kutaka ‘ubuyu’, hatimaye
muda wa kuingia Kiba ukawadia ambapo alitinga na timu yake ya watu
wanne.
Alipofika, Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond kutimba na timu yake kubwa.
Alipofika, Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond kutimba na timu yake kubwa.
Kama ilivyo ada, macho ya waandishi wetu yakaelekezwa kwa Diamond
huku mapichapicha yakiendelea kwa ajili ya kutupia kwenye mitandao ya
kijamii.
Kila msanii aliyefika kwenye ukumbi huo alianza kutoa salamu kwa mtu anayeona anafaa kwake, lakini cha kushangaza mastaa wawili Kiba na Diamond walishindwa kupeana hata mikono huku kila mmoja akiwa ameuchuna na kampani yake.

Hata hivyo, wakati ulipofika wa wasanii kujitambulisha mbele ya
wadau, mastaa hao walitahadharishwa kwamba atakayeanza au atakayekuwa wa
mwisho kujitambulisha haina maana kwamba yeye ndiye mkubwa zaidi
kistaa.
Katika kujitambusha, Kiba ndiye aliyeanza huku kila mtu akitamba kufanya vizuri kwenye kila shoo zitakazofanyika mwaka huu.
Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake.
Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake.
Post a Comment