Akaunti ya Twitter na You Tube ni mojawapo ya mitandao iliyoshambuliwa na watiifu wa Islamic State.
Idara ya upelelezi ya Marekani-FBI inachunguza shambulizi la
mtandao dhidi ya akaunti za Twitter na You Tube zinazomilikiwa na
kitengo cha uongozi wa kijeshi cha Marekani ambacho kinafuatilia
mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Marekani kwa kundi la Islamic
State nchini Irak na Syria.
Washambuliaji ambao walisema ni wafuasi watiifu wa Islamic State kwa
muda mfupi walishambulia akaunti hizo siku ya jumatatu na kuwatishia
wanajeshi wa Marekani kwa ujumbe unaosomeka “tunakuja, angalia nyuma.
ISIS”.
Jumbe nyingine zinajumuisha nyaraka kwenye tovuti ambazo zilikuwa
zimeonekana zikiwa na namba za simu na dazeni za anwani za barua pepe
na anwani za majumbani mwa maafisa wa jeshi la Marekani.
Pia walionyesha kile kilichoonekana kuwa uvujaji wa ramani za kijeshi za China na Korea kaskazini.
إرسال تعليق