Fursa na changamoto katika mkataba wa EPA

Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeingia katika hatua mpya baada ya kusaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara (Epa) na nchi za Jumuiya ya Ulaya.
Hatua hiyo inatokana na mazungumzo yaliyochukua miaka 12 hadi kufikia ukomo wake hivi karibuni.
Mkataba huo unagusa moja kwa moja maisha ya kawaida ya wananchi wa ukanda huo katika masuala mbalimbali na baada ya kusainiwa mwezi Oktoba mwaka 2014, nchi hizo zinalazimika kujipanga upya ili ziweze kufaidi fursa zitakazotokana na utekelezaji wake.
Chanzo cha mkataba
Chimbuko la mazungumzo yaliyozaa mkataba huo linaanzia mwaka 1957, wakati nchi za Jumuiya ya Ulaya zilipoweka sera ya pamoja ya mambo ya nje ya kusimamia masuala ya maendeleo kwa nchi za Kiafrika ambazo nyingi wakati huo zilikuwa bado ni makoloni.
Baada ya nchi nyingi kupata uhuru miaka ya 1963, Jumuiya ya Ulaya iliibuka na aina mpya ya ushirikiano ulioitwa ‘Younde Convention’ uliozishirikisha nchi zilizopata uhuru ili zipate misaada na utaalamu.
Mwaka 2000 ikaonekana kuwa makubaliano baina ya nchi hizo hayakidhi mahitaji ya wakati huo, hivyo kukahitajika makubaliano mapya ambayo yangezingatia mambo mengi zaidi ya misaada. Hatimaye baada ya miaka 14 nchi hizo zikasaini mkataba mpya wa ushirikino.
Kimsingi, mkataba huu ukisharidhiwa na nchi husika, ni hatua ya mwisho ya kufungua mlango wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Ulaya na nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
Fursa zilizopo
Akizungumzia fursa zilizopo katika mkataba na utekelezaji wake, balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dk Diodorus Kamala anasema kuwa bidhaa za Afrika Mashariki zitaanza kuingia Ulaya bila kodi.
Anasema kwa utaratibu huo pia baadhi ya bidhaa kutoka Ulaya zitaanza kuingia kwenye ukanda huo bila kutozwa kodi na katika baadhi ya bidhaa kodi ikiondolewa taratibu kwa muda wa miaka 25.
Dk Kamala ambaye pia ni Mwenyekiti wa mabalozi wa Afrika Mashariki katika Jumuiya ya Ulaya, anasema kuwa makubaliano mapya yatalinda sekta ya kilimo na bidhaa zake na kuwa suala hilo halifutwi na makubaliano mapya

Post a Comment

Previous Post Next Post