Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeingia katika hatua mpya
baada ya kusaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara (Epa) na nchi za
Jumuiya ya Ulaya.
Hatua hiyo inatokana na mazungumzo yaliyochukua miaka 12 hadi kufikia ukomo wake hivi karibuni.
Mkataba huo unagusa moja kwa moja maisha ya
kawaida ya wananchi wa ukanda huo katika masuala mbalimbali na baada ya
kusainiwa mwezi Oktoba mwaka 2014, nchi hizo zinalazimika kujipanga upya
ili ziweze kufaidi fursa zitakazotokana na utekelezaji wake.
Chanzo cha mkataba
Chimbuko la mazungumzo yaliyozaa mkataba huo
linaanzia mwaka 1957, wakati nchi za Jumuiya ya Ulaya zilipoweka sera ya
pamoja ya mambo ya nje ya kusimamia masuala ya maendeleo kwa nchi za
Kiafrika ambazo nyingi wakati huo zilikuwa bado ni makoloni.
Baada ya nchi nyingi kupata uhuru miaka ya 1963,
Jumuiya ya Ulaya iliibuka na aina mpya ya ushirikiano ulioitwa ‘Younde
Convention’ uliozishirikisha nchi zilizopata uhuru ili zipate misaada na
utaalamu.
Mwaka 2000 ikaonekana kuwa makubaliano baina ya
nchi hizo hayakidhi mahitaji ya wakati huo, hivyo kukahitajika
makubaliano mapya ambayo yangezingatia mambo mengi zaidi ya misaada.
Hatimaye baada ya miaka 14 nchi hizo zikasaini mkataba mpya wa
ushirikino.
Kimsingi, mkataba huu ukisharidhiwa na nchi
husika, ni hatua ya mwisho ya kufungua mlango wa ushirikiano wa
kibiashara kati ya Ulaya na nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
Fursa zilizopo
Akizungumzia fursa zilizopo katika mkataba na
utekelezaji wake, balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dk Diodorus Kamala
anasema kuwa bidhaa za Afrika Mashariki zitaanza kuingia Ulaya bila
kodi.
Anasema kwa utaratibu huo pia baadhi ya bidhaa
kutoka Ulaya zitaanza kuingia kwenye ukanda huo bila kutozwa kodi na
katika baadhi ya bidhaa kodi ikiondolewa taratibu kwa muda wa miaka 25.
Dk Kamala ambaye pia ni Mwenyekiti wa mabalozi wa
Afrika Mashariki katika Jumuiya ya Ulaya, anasema kuwa makubaliano mapya
yatalinda sekta ya kilimo na bidhaa zake na kuwa suala hilo halifutwi
na makubaliano mapya
إرسال تعليق