Muigizaji wa Nollywood, Genevieve Nnaji amesema si rahisi yeye kujiingiza katika ndoa
kutokana na ukweli kuwa hicho si kitu rahisi kama wengi wanavyofikiri.
Kwa muda mwingi muigizaji huyo
mwenye mafanikio lukuki amekuwa akiwaacha watuy mdomo wazi kwa kutojua sababu
za yeye kutofunga ndoa.
Binti huyo ambaye mwaka huu
anakuwa na miaka 36 alisema kwamba pamoja na haja ya kuwa na ndoa yeye
anafikiri kuwa ndio si mahala pa kutania na si jambo rahisi.
Akizungumza na Vanguard, alisema:" Kama nitaolewa ninataka kukaa katika
ndoa hiyo na kuendelea na ndoa si jambo rahisi. Inamaananisha kwamba wewe na
mwenzako mkoa pamoja mnazungumza lugha moja.”
“Inamaananisha kwamba umempata
ubavu wako kwa sababu ni lazima uwe tayari kuvumilia mambo mengi magumu ambayo
hakika yatakuja katika ndoa na lazima ujifunze kusamehe,”
alisema binti huyo.
Genevieve Alisha fikiriwa kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki D’banj
baada ya kuonwa pamoja mara kadhaa na pia alitokea kwenye video yake ya wimbo
wa “Fall in love”.
Genevieve Nnaji aeleza kisa cha kuendelea kuwa singo
Hisia
0
Tags
ENTERTAINMENT

Post a Comment