Genevieve Nnaji aeleza kisa cha kuendelea kuwa singo

Muigizaji wa Nollywood, Genevieve Nnaji  amesema si rahisi yeye kujiingiza katika ndoa kutokana na ukweli kuwa hicho si kitu rahisi kama wengi wanavyofikiri. Kwa muda mwingi muigizaji huyo mwenye mafanikio lukuki amekuwa akiwaacha watuy mdomo wazi kwa kutojua sababu za yeye kutofunga ndoa. Binti huyo ambaye mwaka huu anakuwa na miaka 36 alisema kwamba pamoja na haja ya kuwa na ndoa yeye anafikiri kuwa ndio si mahala pa kutania na si jambo rahisi. Akizungumza na Vanguard, alisema:" Kama nitaolewa ninataka kukaa katika ndoa hiyo na kuendelea na ndoa si jambo rahisi. Inamaananisha kwamba wewe na mwenzako mkoa pamoja mnazungumza lugha moja.” “Inamaananisha kwamba umempata ubavu wako kwa sababu ni lazima uwe tayari kuvumilia mambo mengi magumu ambayo hakika yatakuja katika ndoa na lazima ujifunze kusamehe,”  alisema binti huyo. Genevieve Alisha fikiriwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki D’banj baada ya kuonwa pamoja mara kadhaa na pia alitokea kwenye video yake ya wimbo wa “Fall in love”.

Post a Comment

أحدث أقدم