HALI YA BANZA STONE INAENDELEA VIZURI - Kurejea Dar kesho mchana



 Hali ya mwanamuziki Banza Stone ambaye yuko Tunduma mkoni Mbeya inaendelea vizuri na anatarajiwa kurejea Dar es Salaam Jumatatu mchana kwa shirikia la ndege la Fast Jet.

Kwa siku mbili zilizopita, hali ya Banza ilikuwa mbaya huku huduma za kimatibabu zikichelewa, lakini kwa msaada wa wasamaria wema baadae mwanamuziki huyo akapelekwa hospitali, hali iliyosaidia kuleta ahueni.
Kwasasa Banza yuko uraiani (kasha toka hospitali) na yupo tayari kwa safari ya kurejea Dar es Salaam.
Taarifa kutoka kwa mdau Deo Mutta ambaye amekuwa akifanya mawasiliano ya mara kwa mara na watu wa Tunduma inasema hivi (inawekwa kama ilivyo bila kupunguza wala kuogeza neon): Ninaomba kutoa taarifa ya hali ya Mgonjwa wetu Ramadhani Masanja Banza Stone Mwalimu wa Walimu. Nimeongea na Banza asubuhi hii anaendelea vyema na yuko Tayari kwa Safari. Mgonjwa ataondoka Mbeya Kesho kwa Fast Jet na kufika Dar es salaam saa nane mchana. Utaratibu wa airport uko kama ifuatavyo. Bwana Hamis Magodoro na Hamis Masanja (Kaka yake Banza watampokea Airport na kumpeleka Nyumbani Sinza na Baadaye Atakwenda kwenye Clinic yake Sinza Palestina. Jana Band ya Utalii Band ilituma shilingi 51,000/= Kwangu kupitia kwa Wadau wawili wa Muziki Jimmy Kamuzora na Benn Kaguo. Pesa hiyo nimempatia Hamsi Magodoro kwa ajili ya KUKODI TAXI kwenda Airport kumchukua Mgonjwa. Ninaomba kuweka mazungumzo yangu ya moja kwa moja kati yangu na Rahim na pamoja na maongezi yangu na Hamis Magodoro. Mazungumzo yangu na Banza Sitayaweka hapa kwa kuwa asilimia kubwa amezungumzia mambo yake BINAFSI KIAFYA ... hivyo Siyo uungwana kuyaweka IN PUBLIC. Naomba kiwasilisha.

Post a Comment

أحدث أقدم