Kwenye Uheard ya leo Jan 9, Soudy Brown amezungumza na Sheikh Sharif ambaye alitoa taarifa kuwa kuna ndoto aliyoota ambayo ni ujumbe kwa Tz, akitolea ufafanuzi ndoto hiyo Sheikh Sharif amesema alipotafsiri ndoto hiyo aliweza kupata mambo saba ambayo yatatokea kwa mwaka 2015.
Baadhi ya mambo aliyotolea tafsiri ni pamoja na kunyesha kwa mvua kubwa itakayoleta mafuriko, chombo
kikubwa kuzama Baharini na kufariki kwa kiongozi mkubwa kati ya wale
waliotangaza nia ya kugombea Urais, ambaye amemtaja kwamba anakubalika
sana ingawa hajajua ni wa chama gani na wala kifo chake kitatokana na
nini.
Sheikh sharif ameseama amewahi kuota mambo kadhaa siku za nyuma ambayo yalitokea ikiwemo Rais Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Kenya, kuzama kwa meli ya Mv Bukoba na yote yalitokea, hivyo ameamua kulisema hili ili watu wachukue tahadhari.
Unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play

إرسال تعليق