Kaitka vikorombwezo viliovyoandamana na tuzo ya Ballon d'Or aliyoshinda Cristiano Ronaldo, mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez akatwaa tuzo ya goli bora la mwaka.
Goli
hilo la James Rodriguez lilipatikana wakati wa michuano ya Kombe la
Dunia ambapo alifunga dhidi ya Uruguay kwa mkwaju mkali wa mita 25.
Alipokea pasi ya kichwa kutoka kwa Abel Aguilar akautuliza kwa kifua kabla ya kuachia shuti kali lililojaa wavuni.
Wengi
walitaraji bao la Robin van Persie alilofunga katika Kombe la Dunia kwa
kichwa cha mbali akiruka mithili ya Superman ndiyo lingekuwa bao bora
la mwaka, lakini kura hazikutosha.
Post a Comment