Cristiano
Ronaldo ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d'Or) 2014 kwa
mwaka wa pili mfululizo akiwatupa Manuel Neuer pamoja na mpinzani wake
mkuu Lionel Messi.
Ronaldo, 29 alitoa mchango mkubwa kwa Real Madrid mwaka uliopita na kuiwezesha kutwaa mataji ya Copa del Rey, Champions League, UEFA Super Cup na Club World Cup.
Ndani
ya msimu ulipita, Ronaldo akafunga magoli 56 katika mechi 51
alizocheza. Tuzo hii ya Ballon d'Or inakuwa ni ya tatu kwa Ronaldo,
mbili akiwa na Real Madrid na moja akiwa na Manchester United.
“Naweza
kumuona mama yangu, familia yangu. Napenda kuwashukuru wote
walionipigia kura. Kocha wangu, wachezaji wenzangu, rais wa klabu
yangu,” alisema Ronaldo wakati akikabidhiwa tuzo hiyo na Thierry Henry.
“Umekuwa
ni mwaka usiosahaulika kwangu. Kushinda tuzo hii, tuzo ya aina hii, ni
kitu cha kipekee na naweza kusema kuwa nataka kuendelea kufanya kazi kwa
kiwango kile kile na kujaribu kushinda mataji zaidi – binafsi na kwa
timu – kwa mama yangu na kwa baba yangu ambaye yuko pale akimtazama
mwanaye.
“Nataka
kuendelea kuwa bora kadri siku zinavyosonga. Napenda kusema kwa Wareno
wote kuwa kamwe sikufikiria kushinda tuzo hii mara tatu katika mazingira
tofauti.
“Lakini
umekuwa ni utashi wangu wa siku zote. Nataka kuwa mmoja wa wachezaji
bora wa miaka yote, hiyo inahitaji vitu vingi kwahiyo nawashukuru wote
jioni hii ya leo.”
Post a Comment