Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limefanikiwa kudhibiti wanachi
waliobeba madumu wakitaka kuiba mafuta baada ya lori la mafuta kuanguna
katika eneo la Mikese mkoani Morogoro.
Dereva wa lori Deogras John hilo akizungumzia tuki hilo la ajali
amesema chanzo cha ajali alikua akijaribu kukwepa mtoto aliekua akivuka
barabara ndipo gari ikapoteza mweleko na kupinduka mara kadhaa ambapo
wananchi walijitokeza na madumu na kuanza kuiba mafuta.
Nao wananchi wa eneo la Mikese katika hali iso ya kawaida
wamelalamikia jeshi la polisi kuwazuia kuiba mafuta na kueleza kuwa
wamefanya kazi ya kumuokoa dereva kwa kumtoa kwenye gari na hivyo
walipaswa kuchukua mafuta kama ujira wao.
- ITV
إرسال تعليق