THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameitumia
Saudi Arabia salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul
Aziz al Saud (90) ambaye alifariki jana, Alhamisi, Januari 22, 2015, na kuzikwa
leo, Ijumaa, Januari 23, 2015 mjini Riyadh.
Katika
salamu zake kwa Mfalme mpya, Mfalme Salman bin Abdul Aziz al Saud, Rais Kikwete
amesema kuwa anaungana na wananchi wa Saudi Arabia na dunia nzima kuomboleza
kifo cha kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Saudi Arabia na
katika siasa za eneo la Mashariki ya Kati kwa jumla na kwa muda mrefu.
Ameongeza
Rais Kikwete: “Katika miaka yote 10 ya utawala wake tokea 2005 na kabla ya hapo
katika miaka mingine 10 wakati anashikilia utawala badala ya kaka yake Mfalme
Fahd aliyekuwa anaumwa, Mfalme Abdullah alithibitisha uongozi wa kuwajibika na
msimamo thabiti wa kutafuta amani katika Mashariki ya Kati na dunia itaendelea
kumkumbuka kwa mchango huo.”
Amesisitiza
Mhe. Rais Kikwete: “Aidha, sisi katika Tanzania
tutaendelea kuenzi juhudi zake kubwa za kujenga na kuimarisha uhusiano wa karibu
kati ya nchi zetu,” amesema Rais Kikwete.
“Kwa
niaba ya wananchi wa Tanzania, Serikali ninayoiongoza na mimi mwenyewe,
nakutumia wewe Mfalme Salman salamu za rambirambi, na kupitia kwako kwa
wananchi wote wa Saudi Arabia kwa kuondokewa na kiongozi wao. Sisi katika Tanzania tunaungana nanyi
kuomboleza na kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya
Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud. Amen.”
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23
Januari,2015

إرسال تعليق