BAADA
ya hivi karibuni kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu,
Maximilian Bushoke, msanii wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’
amefunguka kwamba hahitaji tena mwanaume kwa sasa.
Msanii wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ akipozi.
Akipiga stori na paparazi wetu, Jini Kabula
alisema kutokana na kwamba alikaa kwenye uhusiano wa kimapenzi muda
mrefu na Bushoke na hakuona faida yoyote, anaujutia muda wake na sasa
ameamua kuachana na masuala ya mapenzi na amejikita kwenye kazi zaidi.
Msanii wa Bongo fleva, Maximilian Bushoke.
“Nimegundua kwamba wanaume ni watu wanaonipotezea muda tu maana
nilimsubiri Bushoke muda wote huo lakini alivyokuja Bongo akanipotezea
hivyo nimeamua kujikita kwenye kazi zaidi,” alisema Jini Kabula.
إرسال تعليق