Gazeti
la kila wiki la vibonzo la Charlie Hebdo la ufaransa toleo la kesho
jumatano linatarajiwa kuchapisha kibonzo cha Mtume Mohamed katika ukurasa
wake wa mbele chini ya kichwa cha habari "Yote yameshasamehewa"
Walioona
kibonzo hicho wanasema Mtume Mohammad ataonekana akishikilia bango
lililoandikwa "Je suis Charlie" maneno yenye tafsiri "mimi ni Charlie,
yaliyotumika kuonyesha mshikamano, baada ya shambulizi katika ofisi za
gazeti hilo jumatano wiki iliyopita ambapo wafanyakazi kumi na wawili wa
gazeti hilo waliuawa.
Nakala milioni tatu za gazeti hilo la kesho
tayari zimeshachapishwa tofauti na kawaida ambapo huwa linachapisha
nakala sitini elfu kwa wiki.(BBC)
Post a Comment