Kaya 105 za Waathirika wa mafuriko katika maeneo ya Magole na
Mateteni wilayani Kilosa zimepatiwa msaada wa bati 1,155 kutoka shirika
la kimataifa la SAVE THE CHILDREN yenye thamani ya shilingi milioni 16.5
ambapo kila kaya imeweza kupata bati 14.
Akizungumza wakati wa kukabidhi bati hizo afisa kutoka shirika la
SAVE THE CHILDREN nchini Peter Nyaluke amesema msaada huo utatolewa kwa
waathirika wa kaya 35 kambi ya Magole na kaya 70 kambi ya Mateteni.
Amesema awali walitoa msaada wa Mablanketi,sabuni,Godoro,Sola, na
Mikeka,na baadaye Seti za vyombo vya ndani,,Mbolea,Majembe na Mashoka
kabla ya sasa kuamua kutoa bati.
Akipokea msaada huo,Mkuu wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo amesema
bati hizo zitawalenga waathirika ambao hawajapata kabisa bati,kwani kuna
baadhi yao walishapatiwa bati kutoka serikalini kupitia ofisi ya waziri
mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI,na kanisa na
kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT.
Tarimo amesema bati hizo zitasaidia waathirika hao kujenga nyumba
za kudumu na kwamba mpaka sasa wilaya hiyo imeanza zoezi la upimaji
viwanja kwa ajili ya kuwagawia waathirika walio kwenye kaya 520
waliokumbwa na mafuriko hayo.
- ITV

Post a Comment