Mtu mmoja ambaye hakuweza kufamika mara moja amegongwa na TRENI
katika eneo la kingolwira nje kidogo ya mji wa morogoro na viungo vya
mwili kusambaa zaidi ya mita mia moja.
ITV imeshuhudia askari na wananchi wakiokota vipande vya viungo vya
mwili ikiwemo miguu na mikono na hawakufanikiwa kukipata kichwa
ingawa viungo vingine kama miguu mikono kifua vilipatikana ambapo
wananchi wa eneo la kingolwira wamesema huenda mtu huyo alikua mlevi
alikua anavuka reli usiku bila kuchukua tahadhari …muhamed juma
,shuhuda .
Station master mkoa wa morogoro Flavian Nyawale amesema
wamekabidhi jeshi la polisi tukio hilo ili kufanya uchunguzi na
kutoa tahadhari kwa wananchi watembea kwa miguu kuach akutembea kando
kando ya reli na kuchukua tahadhari wakati w akuvuka katika makutano
ya reli na barabara ili kuepusha matukio ya ajali zisizo za lazima.
Kamanda wa reli Enginea Simon Chillery akizungumza na ITV kwa
njia ya simu akiwa njiani kuelekea nachingwea amedhibitisha kutokea kwa
tukio hilo na amesema mtu huyo ambaye hakufahamika jina lake
anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 na 40 na uchunguzi wa tukio
hilo unaendelea na kuwakumbusha wananchi kuheshimu sheria za reli kama
ilivyo sheria za barabarani kwa watembea kwa miguu na wanaendesha
vyombo vya moto wanapovuka reli.

Post a Comment