ZILE tuzo kubwa zinazoandaliwa na shirikisho la filamu
Tanzania, lipo katika hatua za mwisho kabisa baada ya kukamilika taratibu zote,
hivyo kwa wale washiriki wanakumbushwa kuwakilisha fomu za ushiriki wa tuzo
hizo.
“kwa wale wote
waliochukua FOMU kwa ajili ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha TUZO za Filamu
Tanzania (TAFA), mnapaswa kuzingati tarehe ya mwisho wa kurudisha fomu hizo kwa
Katibu Mkuu wa TAFF kama ilivyoelekezwa, siku ya mwisho ni IJUMAA ya tarehe 2
JANUARI 2015”,anasema Bishop.
Tarehe
rasmi kwa ajili ya utoaji wa tuzo hizo itatajwa baada ya ukusanyaji na mchakato
kukamilika wakati wowote kutoka shirikisho, usipoteze nafasi hiyo adimu kwa
kushiriki na kujipima kupitia kazi yako utakayowakilisha.
إرسال تعليق