Abdul akionyesha kidole kilichokatwa katika tukio hilo.
STORI:ISSA MNALLYKijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Abdul mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akiukaribisha vibaya mwaka wa 2015 baada ya kung’atwa kidole kimoja cha mkono wa kulia mpaka kukatwa.
Tukio hilo la kustaajabisha lilitokea maeneo ya Corner Baa iliyopo Sinza Africa-Sana majira ya saa saba usiku wa kuamkia Jumatatu, Januari 5 ambapo aliyemfanyia kitendo hicho ni kijana ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Akionyesha kidole kilichojeruhiwa.“Unajua jamaa inaonekana alikuja kwa shari, yaani alipocheleweshewa chipsi zake, akaanza kuwaka.
“Hata alipopewa alilalamika kupunjwa, basi ikasababisha hali ya kuzinguana kati ya yule mnunuzi na muuzaji. Hee.. si tukashangaa yule jamaa akamng’ata muuza chipsi kidole kisha akatema kipande,” akaeleza mtoa habari huyo.
Kijana aliyemng'ata mwenzie kidole akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
إرسال تعليق