Mwanamke aliyetengeneza bia ni miongoni mwa waliopoteza maisha
Serikali
nchini Msumbiji imetangaza siku tatu za maombolezo nchi nzima baada ya
zaidi ya Watu 50 kupoteza maisha baada ya kunywa kilevi kinachoelezwa
kuwa na sumu.
Watu hao walikunywa kilevi hicho wakiwa msibani.
Watu wengine kadhaa waliokunywa kinywaji hicho siku ya jumamosi walikimbizwa hospitalini.
Maafisa
wanasema wanaamini kuwa kilevi hicho cha kienyeji kilichotengenezwa kwa
mtama na mahindi kilikuwa na sumu ya nyongo ya mamba wakati
waombolezaji walipokuwa makaburini.
Sampuli za damu za
walioathirika na pombe hiyo pamoja na sampuli za bia zimepelekwa mji
mkuu wa nchi hiyo, Maputo kwa ajili ya uchunguzi.
Mwanamke
aliyetengeneza pombe hiyo sambamba na nduguze ni miongoni mwa
waliopoteza maisha.uchunguzi kuhusu tukio hilo unafanyika.(BBC)

Post a Comment