Kombe la Mapinduzi liwe endelevu

Michuano ya kombe la Mapinduzi imeingia hatua ya nusu fainali huku tukishuhudia baadhi ya timu ambazo zilikuwa zikipewa nafasi kubwa ya kufika mbali au kutwaa kombe la michuano hiyo zikitolewa katika hatua ya robo fainali.
Mashabiki wengi aliipa nafasi kubwa Yanga, Azam na mabingwa watetezi wa kombe hilo, KCC ya Uganda.

Mpaka kufikia hatua ya nusu fainali Nipashe tunaamini michuano ya mwaka huu inaupinzani mkubwa na kwakuliangalia hilo tumeona kwenye hatua ya makundi mpaka robo fainali na sasa inaingia hatua ya nusu fainali.

NIPASHE tunaamini kuwa michuano hii inamsaada mkubwa kwa wachezaji wetu ambao wanapata michezo michache ya kucheza kwa msimu kwenye ligi kuu hivyo kuwepo kwa mashindano haya kunawafanya wachezaji kupata michezo mingi zaidi ya kucheza.

Kama sisi tumetambvua jambo hilo, ni wazi waandaaji wa mashindano haya wameliangalia hilo na kuona umuhimu wake, yapo mashindano mengi ambayo yanaazishwa lakini yanakuwa ya nenda rudi kutokana na kufanyika kwa kipindi fulani na baadae kupotea  na kurudishwa tena baada ya miaka mingi kupita, mfano wake ni mashindano ya kombe la Taifa 'Taifa Cup' ambayo yalikuwapo miaka ya nyuma na baadae kutoewaka kabla ya kurudi tena miaka michache iliyopita, lakini mwaka 2009 yakatoweka tena rasmi.

Mapinduzi Cup  ni mashindano ambayo yanapata umaarufu kila mwaka na yamekuwa yakivuta hisia za mashabiki wa soka nchinina hata nje ya nchi hususani ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Tunashauri mashindano haya yaboreshwe na kuyafanya yenye mvuto zaidi ya hapa na ikiwezekana timu kutoka nje zinazokuja kushiriki michuano hii ziongezwe hili kutoa changamoto zaidi kwa klabu zetu hapa nchini.

Ni wazi kuwa timu zetu zinazopata nafasi ya kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa moja ya changamoto wanazokutana nazo ni upungufu wa michezo mingi itakayowaweka wachezaji katika hali nzuri kiushindani.

Ligi kuu Tanzania bara inashirikisha timu 14 tu ambapo kwa wastani timu zinacheza michezo 26 pekee kwa msimu mzima na wanapokwenda kushiriki michuano ya kimataifa wanakutana na timu ambazo kwenye ligi zao zinahusisha kuanzia timu 18 na kuendelea na hivyo kuwafanya wachezaji kupata michezo mingi zaidi.

Kwetu hilo halipo na michuano kama Kombe la Mapinduzi iboreshwa na kufanywa kuwa endelevu ili kuwasaidia wachezaji wetu kupata michezo mingi zaidi katika msimu mmoja.

Wakati michuano hii ya Mapinduzi ikielekea ukingoni waandaaji sasa watafakari na kuona ni kwanamna gani wanaweza wakaboresha michuano hii kwa mwakani na moja jambo la kuliangalia ni kuongeza timu za kigeni na pia kuboresha zawadi hili kutoa hamasa kwa timu na wachezaji.

Tunazipongeza timu zote zilizoingia hatua ya nusu fainali na bila ubishi zimeonyesha soka safi na hasa timu zile ambazo hazikupewa nmafasi ya kufika mbali kwenye michuano ya mwaka, timu ka JKU na Polisi zimeonyesha kuwa zinaweza na kujituma kwa kumepelekea kufanikiwa kuzitupa kwenye michuano hiyo timu ‘kubwa’ zilizopewa nafasi ya kufika mbali, timu hizo ni pamoja na Yanga na KCC.

Kabla ya michuano hii kufika tamati kwenye kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya mapinduzi, Nipashe tunawapongeza waandaaji kwa michuano mizuri yenye ushindani.

 
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

Previous Post Next Post