LALLANA WA LIVERPOOL NJE WIKI NNE, kuikosa Chelsea nusu fainali ya Capital One

- kuikosa Chelsea nusu fainali ya Capital One

Liverpool itamkosa kiungo wa kimataifa wa England Adam Lallana kwa mwezi mzima ujao baada ya kuumia mguu.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, alianza kuonyesha kile kilichofanya Liverpool imnunue kwa pauni milioni 25 kutoka Southampton dirisha la kiangazi.

Lallana aling’ara na kufunga katika mechi ya ushindi wa 4-1 Jumatatu iliyopita na akaanza katika mchezo wake wa sita mfululizo wa mechi za kimashindano siku ya Mwaka Mpya dhidi ya Leicester kwenye dimba Anfield.
Hata hivyo Lallana alitolewa dakika ya 55 baada ya kuumia mguu na sasa atakuwa nje ya dimba kwa wiki nne.

Miongoni mwa mechi atakazokosa ni pamoja na mechi mbili za nusu fainali ya Capital One Cup dhidi ya Chelsea (nyumbani na ugenini),

Post a Comment

Previous Post Next Post