Andoni Zubizarreta (pichani juu) ametimuliwa kwenye nafasi yake ya ukurugenzi wa michezo Barcelona huku msaidizi wake Carles Puyol akiachia ngazi.
Zubizarreta ambaye alishika nafasi hiyo tangu Julai 2010, ametimuliwa
na rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu na kuhitimisha tetezi za
kutimuliwa kwake zilizotanda wiki nzima iliyopita.
Taarifa
ya klabu imesema: “Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu ameamua
kusitisha mkataba wa mkurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta.
“Rais kwa niaba ya klabu, anamshukuru Andoni Zubizarreta kwa mchango wake, kujitoa kwake kwa miaka minne iliyopita.”
Barcelona haridhiki na mwendo wa timu na sasa itajadili hatma ya kocha Luis Enrique katika mkutano wa dharura wa bodi ya timu utakaofanyika Jumatano.
Carles Puyol aliteuliwa kuwa msaidizi wa Andoni Zubizarreta mwezi Mei 2014, muda mfupi baada ya kustaafu kusakata soka ndani ya timu hiyo.
Post a Comment