Maajabu ya Zanzibar yamshangaza Tambwe

Unguja.Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe ameyaaga mashindano ya Kombe la Mapinduzi bila kuwa na bao lakini amesema hatayasahau maajabu aliyoyapata katika mechi zao mbili za mwisho.
Akizungumza na gazeti hili jana, Tambwe alisema si jambo geni kwake kupoteza nafasi za kufunga, lakini nafasi ambazo amezipoteza katika mechi mbili za Yanga dhidi ya Shaba katika hatua ya makundi na ule wa robo juzi dhidi ya JKU hatayasahau katika maisha yake.
Tambwe alisema hajui nini kilitokea wakati akimalizia nafasi ambazo alikuwa akizipata uwanjani na hali hiyo haijawahi kumtokea tangu atue nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post